Ripoti kutoka nchini Guinea zinaarifu kuwa hatma ya Rais wa Nchi hiyo Alpha Conde haijulikani baada ya video ambayo haijathibitishwa kumuonesha akiwa mikononi mwa Wanajeshi, ambao wamehutubia Taifa hilo na kusemwa wamefanya mapinduzi.
Wanajeshi wa Guinea wamejitokeza katika runinga ya taifa wakithibitisha kwamba Rais Alpha Conde ameondolewa madarakani, katika hotuba iliyooneshwa kwenye televisheni, Wanaume waliovaa sare za kijeshi, bendera ya Guinea ikiwa nyuma yao wamelihutubia taifa wakijiita Kamati ya Kitaifa ya upatanisho na maendeleo.
MBOWE ATAFUTIWA MASHTAKA ? HATMA YAKE KUJULIKANA LEO “MAFISADI”