Top Stories

Kamanda athibitisha Ofisi ya CHADEMA kuchomwa moto

on

Usiku mwa kuamkia October 13, 2021 watu wasiojulikana wamechoma ofisi za Jimbo za Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo La Tunduma na kuteketeza nyaraka zote za ofisi.

Osia Antony Kibwana ni Katibu wa CHADEMA Jimbo La Tunduma ambae ofisi yake imechomwa moto amesema vitu vilivyochomwa moto ni vitabu, bendera za chama, mihuri na hati mbalimbali za mali za chama ikiwemo viwanja.

Amesema watu waliofanya tukio hilo walivunja mlango na kuingia ndani kisha kuchoma nyaraka hizo hata hivyo ofisi haijateketea kwani kuna watu walipiga simu kwa viongozi nao wakawataarifu Zimamoto na kufanikiwa kuuzima moto.

Akizungumza Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Songwe Isakwisa Lupembe amesema wamesikitishwa na tukio hilo kwani hilo sio tukio la Kwanza miezi mitatu iliyopita vijiwe 6 vya CHADEMA Tunduma vilibomolewa na bendera za chama ziling’olewa.

Hivyo amelaani vikali kuhusu tukio Hilo amemuomba Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe kuhakikisha waliofanya tukio hilo wanakamatwa maramoja na kuwajibishwa kwani vitendo kama hivi vinachangia kuvuruga amani ya Mji wa Tunduma

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe JANETH MAGOMI amethibitisha hi kutokea kwa tukio hilo na amekemea matukio kama hayo na amesema wanaendelea na upelelezi ili kubaini waliohusika na tukio hilo.

GAUNI LA BIBI HARUSI LAWAKA MOTO UKUMBINI DAR, GARI LAO HUMMER LAGONGA

Soma na hizi

Tupia Comments