Top Stories

Kamanda Jonathan Shana afariki dunia Dar es salaam

on

Ni taarifa za msiba wa Jonathan Shana asubuhi hii kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es salaam ambazo zimethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Hospitalini hapo Aminiel Aligaesha.

Aminieli amesema ni kweli Jonathan Shana ambaye aliwahi kuwa Kamanda wa Polisi Arusha amefariki usiku wa kuamkia leo Sept. 16 2020 Hospitalini hapo ambako alikua amelazwa kwa siku 21 ambapo kati ya hizo siku 21 alikua kwenye chumba cha Wagonjwa Mahututi  (ICU) kwa siku 3.

Hii hapa chini ni moja ya video za Marehemu Jonathan Shana wakati wa uhai wake, ilikua ni Mwanza akiwaaga Askari wenzake baada ya kuhamishwa kituo cha kazi na mikoba yake kuchukuliwa na Muliro Jumanne.

Soma na hizi

Tupia Comments