Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: Kamati ya Bunge yaitaka Serikali ilipe madeni Taasisi zake
Share
Notification Show More
Latest News
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo June 3, 2023
June 3, 2023
Picha: DC Halima Bulembo aungana na wakuu wa Idara, ‘Kutekeleza wajibu wao katika Utumishi’
June 2, 2023
Upinzani unashinikiza mageuzi mapya ya uchaguzi
June 2, 2023
Mlipuko wa ugonjwa wa Marburg umekwisha rasmi Tanzania.
June 2, 2023
Nyota wa zamani wa Manchester United Lingard kuondoka Nottingham Forest
June 2, 2023
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Top Stories > Kamati ya Bunge yaitaka Serikali ilipe madeni Taasisi zake
Top Stories

Kamati ya Bunge yaitaka Serikali ilipe madeni Taasisi zake

March 20, 2023
Share
3 Min Read
SHARE

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeitaka serikali kuhakikisha taasisi zilizochini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia kulipwa madeni yao ya muda mrefu ili ziweze kujisimamia na kujiendesha kibiashara.

Baadhi ya taasisi zilizotajwa kuwa na madeni ya muda mrefu na kushindwa kukopesheka ni Shirika la Posta, Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Akizungumza jijini jana Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Seleman Kakoso alisema kuwa ni lazima serikali kuhakikisha inasimamia madeni hayo ili mashirika hayo yaweze kukopesheka na kujiendesha kibiashara.

Kakoso alisema TTCL, Posta, TSN na TBC zina miradi mingi lakini kutokana na madeni makubwa haziwezi kukopesheka na kujiendesha hivyo, waweke mikakati ya kuwasaidia.

Kakoso alishauri serikali ihakikishe mkongo wa taifa unaosimamiwa na TTCL unajiendesha kibiashara ili kuleta mapinduzi katika sekta ya mawasiliano.

“Wizara iangalie namna ya kuongeza bajeti kwa TBC kwani kutokana na bajeti yao haiwezi kwenda kwenye ushindani wa soko la habari lakini katika Chaneli ya Safari haipati chochote na ndio maana wanarudia vipindi kwa sababu hawana uwezo wa kuandaa vipindi vipya kwa kuwa hawana fedha, muone namna ya kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii,” alisema Kakoso.

Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia, Nape Nnauye alisema kuwa mpango wao ni kuhakikisha madeni yote yanalipwa kwani TSN pekee inadai zaidi ya Sh bilioni 11, na tayari wameanza uhakiki wa madeni yanayoweza kulipwa yalipwe na yanayoweza kugeuzwa kuwa mtaji wafanye hivyo.

Nape alisema mchakato wa kuzifanya taasisi hizo kujiendesha kibiashara unaendelea na ndio maana wamewapa TTCL mkongo na kituo cha data wasimamie na kujiendesha.

Pia alisema wamefanya mabadiliko ya sheria ya posta ili kuwafanya waweze kujiendesha kibiashara sambamba na kuwataka kuwa na ubia na taasisi mbalimbali.

“Tumepokea maelekezo ya kamati ya bunge ya kuharakisha mchakato wa taasisi hizo zijisimamie kibiashara. Kuhusu upatikanaji wa huduma za redio mipakani, tumeelekeza TTCL kushirikiana na watoa huduma za redio kuongeza kasi ya upatikanaji wa masafa ya ndani,” alieleza Nape.

Pia alielekeza TTCL na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuweka miundombinu ya mkongo wa taifa kwenye nguzo za za umeme badala ya kufukia ardhini jambo ambalo linaongeza usalama.

You Might Also Like

Picha: DC Halima Bulembo aungana na wakuu wa Idara, ‘Kutekeleza wajibu wao katika Utumishi’

Upinzani unashinikiza mageuzi mapya ya uchaguzi

Mlipuko wa ugonjwa wa Marburg umekwisha rasmi Tanzania.

Nyota wa zamani wa Manchester United Lingard kuondoka Nottingham Forest

Serikali ya Congo na mahakama ya ICC zakubaliana kuimarisha ushirikiano

TAGGED: TZA HABARI
Pascal Mwakyoma TZA March 20, 2023
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article Video: Tazama Polisi wazuia Maandamano nchini Kenya
Next Article Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo March 21, 2023
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo June 3, 2023
Magazeti June 3, 2023
Picha: DC Halima Bulembo aungana na wakuu wa Idara, ‘Kutekeleza wajibu wao katika Utumishi’
Top Stories June 2, 2023
Upinzani unashinikiza mageuzi mapya ya uchaguzi
Top Stories June 2, 2023
Mlipuko wa ugonjwa wa Marburg umekwisha rasmi Tanzania.
Top Stories June 2, 2023

You Might also Like

Top Stories

Picha: DC Halima Bulembo aungana na wakuu wa Idara, ‘Kutekeleza wajibu wao katika Utumishi’

June 2, 2023
Top Stories

Upinzani unashinikiza mageuzi mapya ya uchaguzi

June 2, 2023
Sports

Nyota wa zamani wa Manchester United Lingard kuondoka Nottingham Forest

June 2, 2023
Top Stories

Serikali ya Congo na mahakama ya ICC zakubaliana kuimarisha ushirikiano

June 2, 2023
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?