Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imesema kuwa,itaishawishi serikali itoe fedha kwa wakati ili Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) liweze kukamilisha miradi yake kwa wakati ili iweze kuleta tija kwa Serkiali na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza mara baada ya kamati hiyo kutembelea miradi hiyo jijini Dar es Salaam ,Mwenyekiti wa kamati hiyo,Deus Sangu kuwa,katika kikao kijacho cha Bunge la Bajeti wataendelea kuishawishi Serikali kutoa fedha ili NHC iweze kukamiisha miradi hiyo.
“Tumetembelea miradi Mikubwa ambayo ikikamilika italeta mrejesho kwa Serikali,kama kamati Katika kikao cha Bunge la Bajeti tutaendelea kuishawishi Serikali ili itoe fedha ili miradi hiyo ikamilike”.
Mwenyekiti huyo ametoa pia rai kwa serikali kutoa fursa kwa watanzania waishio nje ya nchi na wageni kushiriki Katika kuwekeza kwenye sekta ya uendelezaji miliki.
Vilevile amempongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa vibali kwa Shirika hilo liweze kukopa na kufanya miradi ya uwekezaji.
Naye Mkurugenzi wa NHC,Hamad Abdallah Hamad ameishukuru kamati hiyo kwa ushauri ambao wamekuwa wakiutoa ndani na nje ya Bunge.
Pia Mkurugenzi huyu ameahidi kumanya Kazi Kwa weledi ili kuleta tija kwa serikali na Taifa kwa ujumla na aliongeza kwamba kwenye miradi hiyo ya nyumba tayari nyumba 60 kati ya 100 zimekwishakupata wanunuaji.