Ni February 20, 2024 ambapo Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza kuu la UVCCM wakiongozwa na Mwenyekiti UVCCM Taifa Ndugu Mohammed Ali Kawaida (MCC).
Watembelea chuo cha VETA Manyara kilichopo katika kata ya Babati Wilaya ya Babati Mjini ambapo alitembelea karakana, madarasa ya kufundishia, maabara na chumba cha TEHAMA, pia alipata wasaa wa kuwasalimia Wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho na kuwapa moyo kuwa Serikali inatambua uwepo wao na inaandaa mazingira mazuri ya Vijana kujiajiri.
Kaimu Mkuu wa Chuo aliwasilisha kero tatu zinazokuwa kikwazo katika utendaji wa chuo hicho ambazo ni uhaba wa madarasa ya kufundishia, karakana pamoja na Mabweni ya Wanafunzi kulala.
Mwenyekiti amekiri kupokea kero hizo na kuwahakikishia kuwa kwa namna VETA hiyo inavyotekeleza nia na dhamira ya Mhe. Rais ya kuwafundisha vijana wetu waweze kujiajiri na Serikali yetu ilivyo sikivu kero hizo zitafanyiwa kazi na VETA hiyo iendelee kuwa ya mfano Tanzania pamoja na nje ya Tanzania.