Usalama wa mtandao ni ulinzi wa mifumo ya kompyuta na mitandao dhidi ya mashambulizi na wahalifu ambayo yanaweza kusababisha kufichuliwa kwa taarifa bila ruhusa, wizi, au uharibifu wa vifaa, programu, au taarifa za kompyuta, pamoja na usumbufu au kupotoshwa kwa huduma zinazotolewa.
Usalama wa mtandao ni mojawapo ya changamoto kubwa zaidi katika ulimwengu wa sasa, kutokana na umuhimu wa mifumo ya habari na jamii zinazotumika.
Unapotumia mtando vibaya kwenye usambazaji wa taarifa au kuutishia umma kwa taarifa potofu kunaweza kuchangia uzimwaji wa mtandao hasa kwenye matukio muhimu kama vile uchaguzi nakadhalika.
Kuzimwa huku kwa mtandao kunaadhiri maisha ya wananchi kikazi, kimasomo, kibiashara na pia katika mahusiano.
Imeonekana wazi kwamba kuzimwa kwa mtandao kunaathiri pakubwa maisha ya wananchi.
Mfano :Kabla uchaguzi wa Urais Oktoba 28 2020, mashirika yanayohusika na mawasiliano yalichukua hatua mbalimbali kukatiza haki za kidijitali za wananchi wa Tanzania kwa kuzima mtandao kama njia ya kuzuia usambazaji taarifa potofu za matokeo nk. lakini hii iliathiri pakubwa waandishi na watoaji wakubwa wa habari nchini hii iliangaziwa kwenye mitandao kama Twitter, WhatsApp na Telegram.
Kuzimwa kwa mtandao kuliathiri uwezo na haki ya msingi ya kupata habari mbalimbali katikati ya wakati muhimu wa uchaguzi.
hivyo inatupasa kuwa makini na taarifa tunazozisambaza kwenye mitandao na kusimama kwa pamoja katika ushiriki wa kutoa elimu juu ya matumizi sahii ya mtandao na haki ya kupata taarifa sahihi kwa wakati sahihi.
Kupitia kampeni ya #KeepItOn kampeni ambayo ihusisha zaidi ya mashirika 220 ikiwemo #Zaina foundation ambayo imeungana kupiga vita uzimaji wa mtandao kupitia kutoa elimu, msaada wa kiteknolojia, msaada wakisheria na kadhalika ipo tayari kukuelimisha wewe mtumiaji namna sahihi ya kuutumia mtandao na kupata faida kupitia njia mbalimbali.
#KeepItOn