Tume ya Uchaguzi nchini Uganda imesimamisha kampeni katika maeneo ya mijini yenye idadi kubwa ya watu kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19.
Wilaya zilizozuiwa kufanya Kampeni ni Mbarara, Kabarole, Luwero, Kasese, Masaka, Wakiso, Kabarole, Jinja, Kalungu, Kazo and Tororo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo, Simon Mugenyi kampeni zimepigwa marufuku katika maeneo hayo hadi itakapotangazwa tena mara baada ya tume kukutana na wataalamu wa afya siku za hivi karibuni ili kupata ufumbuzi wa tatizo hilo.