Kampuni 15 kutoka nchini Misri zimekuja nchini Tanzania kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu wa wafanyabiashara wa Watanzania.
Akizungumza leo Mei 17 ,2021 wakati wa maonesho madogo ya bidhaa za kampuni hizo, Muwakilishi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Edwin Rutageruka amesema lengo na dhumuni ya kampuni hizo kuja nchini ,ni kutaka kuona mazingira ya kibiashara nchini ili kupanua wigo wa soko la bidhaa baina ya nchi hizo mbili.
Amesema wafanyabiashara hao kupitia kampuni zao wamekuja na bidhaa mbalimbali ikiwemo dawa binadamu, mbolea pamoja na kemikali mbalimbali.
Aidha amesema licha ya kampuni hizo kutaka kujua watawezaje kuja kufanya biashara yao hapa Tanzania ni kwamba Watanzania wanaweza kunufaika sana ,hivyo ni wakati wa kuchangamkia fursa kwa kuzalisha kahawa ,na kupeleka Misri.
Amezitaka kampuni zinazojishughulisha na utengenezaji vifungashio nchini kuchukua au kupata ujuzi wa kutengeneza vifungashio vilivyo bora na imara kwa maana wenzetu egypt vifungashio vyao viko vizuri na kwa ubora zaidi.
Ameziomba kampuni hizo kutoka Misri kuja kuwekeza nchini kwenye maeneo ya viwanda vya kutengeneza nguo.” Kama tunavojua upatikanaji wa ngozi hapa Tanzania ni wakutosha hivyo si mbaya kama wakifungua kiwanda cha uzalishaji mikoba au mabegi,viatu vya ngozi ,na hivyo kunufaika sote.”
Pia amewataka vijana kuchangamkia fursa ya kuwa hata mabalozi wa kusambaza bidhaa hizo.