Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (Yas)imeendelea kutambulisha mabadiliko yaliyotokea katika kampuni hiyo pamoja na huduma zake kwa kanda ya Kaskazini baada ya kufanya mabadiliko ya Chapa yake mpya ya Yas ambayo awali ilijulikana kama Tigo.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Arusha, Afisa Mkuu wa Biashara Yas,Isack Nchunda alisema tangu mabadiliko hayo yafanyike Novemba 26,2024 kampuni hiyo imekuwa na mwendelezo wa kutambulisha chapa yake mpya inayoenda sanjari na maboresho makubwa katika ulimwengu wa kidigitali unaotoa matumani Mapya
“Tupo hapa Kutambulisha Mabadiliko ya Chapa yetu ya Yas, Kama mnavyofahamu Novemba 26 Mwaka jana 2024, kampuni yetu iliyofanyakazi kwa zaidi ya miaka 30 ilikuwa ikitukima jina la Tigo pamoja na Tigo Pesa, tumefanya mabadiliko hayo na sasa ni Yas na Tigo Pesa Ni Mixx by Yas”
Alisema mabadiliko hayo ya Chapa ya Yas ni hisia chanya yenye matumani mapya kwa wateja kutokana na uwekezaji mkubwa wa Mtandao Tanzania ambapo kwa sasa Yas inapatikana nchi nzima kwa Mtandao mpana wenye kiwango cha masafa ya 4G na 5G ukiwa ni Mtandao bora zaidi kwa huduma unaotambuliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA.