Baadhi ya makampuni makubwa ya nishati barani Ulaya yanapanga kutumia mfumo mpya wa malipo kwa usambazaji wa gesi ya Urusi uliopendekezwa na Kremlin gazeti la Financial Times liripoti siku ya Alhamisi.
Vyanzo vya habari vililiambia gazeti hilo kuwa wasambazaji wa gesi nchini Ujerumani, Austria, Hungary na Slovakia wanapanga kufungua akaunti za ruble katika benki ya Gazprombank nchini Uswizi.
Walisema kuwa mazungumzo kati ya wanunuzi wa Uropa na wasambazaji wa gesi wa Urusi Gazprom yameongezeka kadri muda wa malipo unavyokaribia.