Michezo

Kane hataki kuongea na Kocha mpya wa Spurs kwa sasa

on

Nahodha wa England na club ya Tottenham Hotspurs ya England Harry Kane ameweka wazi msimamo wake kuwa hajafanya mazungumzo na hataki kufanya mazungumzo kwa sasa na Kocha npya wa Tottenham Hotspurs Nuno Espirito.

Kane ameyasema hayo kwa nia njema ya kuelekeza nguvu zake katika kuisaidia England kusaka Ubingwa wa Euro 2020, Kane anahusishwa kuondoka na Spurs na idandaiwa kuwa Kocha Nuno kampigia kumshawishi abakie Spurs.

“Niko na England kwa sasa na shabaha yangu iko hapa (Euro2020), natumai tumebakiza wiki moja michuano kumalizika, (Nuno) ni kocha mzuri alifanya kazi kubwa akiwa na Wolves na kuifanya iwe na mchezo mzuri naimani  tutawasiliana baada ya mashindano kumalizika”>>>> Kane

Nuno ametangazwa wiki iliyopita kama Kocha mpya wa Tottenham na sasa intajwa kuwa na kazi ya kumshawishi Harry Kane asiondoke Spurs, Kane anahusishwa kuwa mbioni kujiunga na Man City.

Soma na hizi

Tupia Comments