Rapper wa Marekani Kanye West (44) sasa anatambulika kisheria kwa jina la ‘Ye’ baada ya Jaji kukubaliana na ombi lake la kubadilisha jina.
Ye ambae sasa hivi yupo kwenye headlines na staili yake mpya ya kunyoa nywele kama kaparurwarurwa amekubaliwa kubadili jina na Jaji Michele William wa Mahakama Kuu Los Angeles ambapo kwenye maombi yake, Ye alitaja sababu za kubadili jina lake kuwa ni sababu binafsi.
Mabadiliko ya jina hili sio kitu kipya kwa Mashabiki wa Kanye kwasababu ni rahisi kwao kukumbuka kwamba Rapper huyo alitaka aitwe Ye tangu mwaka 2018 ambapo tayari kwenye account zake za social media Kanye ameliweka jina la YE.
HISTORIA YA KUSISIMUA YA DJ JOOZEY “NIMEISHIA LA SABA, NIMEPIGA DEBE KARIAKOO”