fB insta twitter

Kanye West: “Sitaki usumbufu wala kuombwa chochote kwa sasa”… kwanini!? Majibu haya hapa!

on

Kanye West ni miongoni ya wasanii walioweka headlines kubwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter baada ya tweets zake mbili za mwisho kuweka attention kubwa kwenye social media, pamoja na kwenye websites mbalimbali za Marekani.

Kwa muda sasa Kanye West amekuwa busy akijitahidi kukamilisha album yake ya saba SWISH, licha ya uzinduzi wa album hiyo kupigwa kalenda kila mara bila sababu zozote kuwekwa wazi… Kama wewe ni mfuatiliaji wa Kanye basi ikufikie kuwa rapper na producer huyo amewaomba watu wamuache awe free mpaka pale atakapo kamilisha album yake mpya!

weee2

Je hii inawezekana ikawa sababu ya kwa nini Kanye West amekuwa akisogeza mbele tarehe ya uzinduzi wa album yake mpya? Kwa mujibu wa tweets zake za siku mbili zilizopita (12 December 2015) ni wazi kuwa Kanye anakwama na kushindwa kukamilisha album hiyo kutokana na watu kumuomba rapper huyo ‘favors’ nyingi.

weee3

Kanye West.

Kupitia page yake ya Twitter, Kanye West amewaomba watu wamuache kwa sasa na wasimsumbue kwani yupo busy anakamilisha mambo yake…

>>>”Nipo nakamilisha album yangu mpya na collection yangu mpya pia… simaanishi vibaya… ila nawaomba MSINIOMBE KITU CHOCHOTE MPKA NTAKAPOKUWA NIMEKAMILISHA ALBUM YANGU…“<<< aliandika Ye kupita account yake ya twitter @KanyeWest.

Hizi ni tweets mbili za Kanye akiomba aachwe kwa sasa:

west2

>>> “Nakamilisha album yangu na collection yangu ijayo… ” <<< @KanyeWest.

west

>>> “simaanishi ubaya kwa mtu yoyote… Nawaomba MSINIOMBE KITU CHOCHOTE MPAKA NTAKAPOKUWA NIMEKAMILISHA ALBUM YANGU” <<< @KanyeWest.

Usijali Kanye fanya yako!

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FBInstagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

 

Soma na hizi

Tupia Comments