Habari za Mastaa

Kanye West haishiwi vioja! Haya ni mengine kutoka kwake…+ (Video).

on

CEO wa lebo ya G.O.O.D Music Kanye West hivi karibuni alifanya interview na SHOWstudio, interview ambayo iligusia mada nyingi ikiwemo, ubaguzi wa rangi Marekani, ubunifu wake wa mitindo na mavazi pamoja na muziki, na shauku yake kuitwa ‘genius’ na mambo mengine mengi.

YAE

Alipoulizwa kuhusu mchango wake kwenye muziki, Kanye West alishare mawazo yake kwa kile anachokiita ‘muziki wa sasa hivi’ Marekani akidai chochote kile unachokisikia sasa hivi kwenye muziki yeye alishakifanya miaka 10 iliyopita!

YAE3

>>> “Vitu vingi ambavyo vinatamba na kupendwa sana sasa hivi ukivifuatilia utagundua vyote nilishavifanya miaka 10 iliyopita. Unaweza ukakaa na kuchambua mwenyewe… nafikiri hii inanipa message kubwa sana, nafikiri dhamira yangu duniani ni kubwa zaidi… kwahiyo ukisikia kitu kinachofanana na kitu chochote alichowahi kufanya Kanye West basi  ujue hiyo itakuwa muendelezo wa album mpya kwangu pia.” <<< Kanye West.

YAE4

Akaongezea kwa kuwataja baadhi ya wasanii waliomshawishi kufanya muziki wakiwa Jay Z, A Tribe Called Quest na Dre. DreKanye wala hakuishia hapo mtu wangu aliendelea kujisifia na kusema ni jinsi gani ambayo yeye ni ‘genius’ yani jinsi gani ambavyo ana akili kupita kiasi licha ya watu kumuona tofauti!

YAE2

>>> “mara nyingine huwa nahisi mimi ni ‘a genius’ na huwa najiita hivyo mara nyingi kwasababu kama sitajiona hivyo basi watu wanaishia kuniita ‘celebrity’, ‘nigger’ na vingine na mimi sio hivyo vitu. Wakati mwengine naitwa ‘rapper’ na wakitumia majina haya yote sio kwamba wanayatumia kwa namna na mawazo chanya, licha ya kuwa majina hayo yote yanaweza kutumika kwa nia nzuri kabisa… kwahiyo mwisho wa siku naona ni bora kwa mimi kuamua niitwe nani…” <<< Kanye West.

Unaweza kumsikia Kanye West kwa marefu zaidi kwenye interview yake na SHOWstudio, kwenye hii video hapa chini.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM, TWITTER,FB, YOUTUBE

 

Soma na hizi

Tupia Comments