Habari za Mastaa

Wasanii na matumizi yao ya pesa, haya ndio malipo ya kinyozi wake Kanye West kwa mwaka!

on

Siku zote rapper na Mkurugenzi wa lebo ya G.O.O.D Music, Kanye West amekuwa akionekana kama mtu mkorofi mwenye maneno mengi. Lakini wengi wetu tunaujua upande mmoja tu wa Kanye West, ukorofi na vituko vyake lakini vipi kuhusu upande wake wa pili?

Inawezekana unajua ama hujui vingi sana kuhusu mtu wetu Kanye, licha ya vitendo vyake vingi siku hizi kuweka headlines msanii huyo wa muziki wa HipHop ameingia kwenye headlines nyingine za wasanii wenye matumizi yaliyopitiliza viwango!

YEBARBER4

Je unafahamu kuwa Kanye West anamlipa kinyozi wake dola $500 kwa wiki?! Hii kwa pesa ya nyumbani inagusa kitu kama Tzs milion 1 na laki moja! Yes, mtu wangu Kanye kwa wiki anatumia zaidi ya milioni moja kunyoa nywele tu!

Uthibitisho wa matumizi haya ya pesa yalitoka kwenye interview ya baba yake Rihanna, Ronald Fenty na jarida la Heat Magazine ambapo ndani yake mzee huyo aligusa jinsi ambavyo alikuwa miongoni ya watu waliopata shavu la kusafiri na Kanye kwenye tour ya mwanae mwaka 2010.

YEBARBER5

Kanye West na kinyozi wake IBN Jasper.

>>> “ Inashangaza sana… anamlipa kinyozi wake dola $500 kwa wiki na muda wowote akitaka kunyoa anamlipa hela hiyo… sielewi ana nywele kiasi gani kichwani mpaka awe ananyoa kila wiki na kutoa kiasi hicho cha pesa kwa kinyozi wake, japo nakubali kwa asilimia mia kuwa Kanye anapenda kuonekana smart kichwani, hata akifuga afro litakuwa ni afro fulani smart kweli… lakini kwa malipo hapo, mimi naona kama ni kitu cha kushangaza sana!” <<< Ronald Fenty.

YEBARBER7

Licha ya IBN Jasper kuwa kinyozi wa Kanye West, Jasper pia ni rafiki mkubwa wa utotoni wa rapper huyo.

Huo ni ushuhuda wa baba yake Rihanna uliotokea miaka mitano iliyopita, kinyozi wa Kanye West anaitwa Ibn Jasper na kwa mujibu wa baadhi ya mitandao kama Complex wa Marekani vinyozi wa mastaa hutengeneza pesa ndefu kwa kazi yao kulingana na mahitaji ya msanii wake, kwa pesa hiyo tu kwa wiki, kinyozi huyo anaingiza kitu kama dola $182,500 kwa mwaka ambayo kibongo bongo hii ni zaidi ya Tzs milion 400!

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

 

Soma na hizi

Tupia Comments