Habari za Mastaa

Kanye West ameamua kutoa zawadi hii kwa Rais Barack Obama…!

on

Baada ya Rais wa Marekani, Barack Obama kumpatia Kanye West dondoo za namna ya kuwa Rais, wawili hao mida hii walikuwa jijini San Francisco kwa ajili ya kushiriki kikamilifu kwenye ‘Democratic National Convention Fundraiser’… baada ya shughuli nzima kuisha Kanye akaona haitakuwa poa sana kumuacha Rais aondoke mikono mitupu!

Kutokana na tweet ya Kim Kadarshian , inaonekana Rais Barack Obama amejipatia vitatu vya bure kabisa vya ‘Yeezy Boost 350’  kutoka kwenye collection mpya ya Kanye West iliozinduliwa siku chache zilizopita jijini New York!

KIMWEST2

Tweet iliyowekwa na Kim Kadarshian inaonyesha mabox mawili ya boots za Adidas yakiwa na signature ya Kanye West kwenye kila box na vinoti vilivyoandikwa “Obama” kwenye kila box…Tweet ya Kim Kadarshian ilikuwa inasema;“Special delivery #yeezys”

KIMWEST

Kwa muonekano wa mambo inaonekana Rais Obama sasa hivi atakuwa na pair za kipekee kabisa kwenye kabati lake la viatu, au pengine hii ni namna ya Kanye West kuonyesha shukrani kwa Rais Obama kwa ushauri aliompatia!

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM, TWITTER, FB, YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments