Mix

Umesikia kuhusu ‘Karantini’ ya Marekani kulinganishwa na jela? Stori iko hapa

on

Nesi IISaa chache baada ya New York na New Jersey kutangaza utaratibu mpya wa kuwaweka karantini wauguzi waliotoka nchi za ukanda wa Afrika Magharibi, muuguzi mmoja ambaye amewekwa karantini New Jersey amelalamikia kitendo hicho kuwa kinawafanya madaktari na wauguzi kuwa kama wafungwa.

Muuguzi huyo Kaci Hickox ameripotiwa na The Dallas Morning News kwamba baada ya vipimo kuonesha hana maambukizi ya Ebola, agizo la hospitali limemtaka aendelee kukaa karantini kwa kipindi cha siku 21.

Agizo la kuwaweka karantini kwa siku 21 wauguzi na madaktari kutoka Afrika Magharibi limezua mijadala maeneo mbali mbali Marekani.

Agizo hilo lilitolewa na magavana wa New York na New Jersey baada ya Daktari mmoja, aliyerejea New York akitokea Afrika Magharibi kukutwa na maambukizi ya virusi vya Ebola.

 

Tupia Comments