Habari za Mastaa

Licha ya yote, Karrueche Tran ameyasema haya kuhusu Chris Brown na mahusiano..!

on

Model na mwigizaji wa movie Marekani, Karrueche Tran alipata umaarufu mkubwa sana baada ya ukaribu wake na msanii wa R&B Marekani Chris Brown kuweka headlines kubwa sana, na baada ya kuficha kwingi hatimaye wawili hao waliiambia dunia nzima kuwa wao ni wapenzi.

KARRUECHE2

Baada ya miaka mitano ya kuwa pamoja, mapenzi kati ya Chris Brown na Karrueche Tran yalifika mwisho mwanzoni wa mwaka 2015 baada ya model na actress huyo kujua kuwa Chris ana mtoto na mwanamke mwengine… Imepita miezi tisa toka haya yote yatokee, je Karrueche ana yapi ya kusema juu ya mpenzi wake wa zamani Chris Brown?

KARRUECHE3

Karrueche Tran na mpenzi wake wa zamani, Chris Brown.

Kwenye interview aliyofanya siku chache zilizopita na jarida la Kontrol Magazine, Karrueche Tran alisema haya kuhusu msanii huyo na maamuzi ya yeye kutokuwa kwenye mahusiano yoyote ya kimapenzi kwa sasa…

>>> “ Bado sijaanza kuwa available kwa ajili ya kukaribisha mahusiano yoyote ya kimapenzi, nadhani bado sijawa tayari kisaikolojia kuanza kuwa na mpenzi baada ya Chris, inahitaji utayari wa vitu vingi ili kuanza kuwa muwazi wa kuhitaji mpenzi… nadhani watu wengi ninaokutana nao bado wana wasiwasi na drama zilizopo kati yangu na Chris. Siwezi kuwalaamu kwani nilijitoa sana kwa Chris na mpaka leo bado naumizwa na ukweli wa yeye kuamua kuzaa na mwanamke mwengine…” <<< Karrueche Tran.

KARRUECHE4

Japo Chris Brown ameendelea na maisha yake akiwa ameweka nguvu nyingi kwenye muziki na kwa mtoto wake wa kike Royalty, lakini inaonekana Karrueche Tran ana safari ndefu sana mpaka kuja kumsahau na kumtoa moyoni Chris Brown.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments