Michezo

Hivi ni viatu na gloves maalum Juma Kaseja katengeneza kwa ajili yake(Picha)

on

Golikipa mkongwe kwenye gemu la soka Tanzania Juma Kaseja, ni mchezaji wa soka wa kiwango cha juu kwa muda mrefu na baada ya kukaa nje ya lango kwa muda mrefu staa huyo wa soka  amerejea tena kwenye soka.

Juma Kaseja anarejea uwanjani akiwa chini ya klabu mpya ya soka ‘Mbeya City’ na tunategemea kumuona kwa mara ya kwanza uwanjani msimu ujao baada ya kuwa nje ya lango kwa zaidi ya miezi sita .

kaseja

Katika maandalizi ya kurudi langoni Kaseja ametengeneza viatu maalum kwa ajili yake hivyo usishangae kumuona akiwa langoni na viatu vyenye jina lake Kaseja Coper 1 pamoja na gloves.

Kwenye exclusive na millardayo.com, Juma Kaseja hakuwa tayari kuzungumzia gharama alizoingia kutengeneza vifaa hivyo ila amegoma kutaja gharama aliyotumia kutengeneza viatu hivyo.

kaseja

Kaseja amewahi kuitwa ‘Tanzania One’ kutokana na umahiri wake akiwa langoni, je huu ni mpango wake wa kufanya biashara ya vifaa vya michezo kwa kutumia jina lake ama ni kwa ajili ya matumizi yake binafsi?

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

 

Tupia Comments