Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe Patrobas Katambi amewaomba viongozi wa dini na watanzania kwa ujumla kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani katika juhudi anazozionesha kuitumikia nchi na kuleta ustawi wa maendeleo endelevu.
Katambi ameyasema hayo katika halfa ya Iftari iliyoandaliwa kwa viongozi wa dini jimbo la shinyanga mjini ambapo aliongeza kuwa Mh. Rais analo jukumu kubwa la kuwaletea watanzania maendeleo hivyo viongozi wa dini pamoja na watanzania wote wanapaswa kumuombea ili kufikia adhima hiyo.