Shirika la Viwango nchini TBS limeendelea kutoa elimu kwa Wananchi juu ya kuzingatia alama za ubora na matumizi ya bidhaa zilizothibitishwa na TBS.
Akitoa elimu hiyo Afisa udhibiti ubora Kanda ya Magharibi (TBS) Bw. Hassan Hassan amewataka kutumia bidhaa zenye alama ya ubora na kwa wajasiriamali kujitahidi wapate alama ya ubora katika bidhaa zao kwa manufaa ya wao na walaji.
Ametoa elimu hiyi kwa wajasiriamali waliotembelea banda la TBS kwenye Maonesho ya tatu ya Wiki ya Mwanakatavi yanayoendelea katika viwanja vya Azimio Mpanda, Mkoani Katavi.