Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ameivalia njuga barabara ya kiwango cha lami ya kilomita 25 kutoka Mbulu mjini ambayo inapita Hydom hadi Singida inayojengwa kwa zaidi ya shilingi bilioni saba baada ya kubaini mradi huo kusuasua kutokana mkandarasi kutolipwa fedha za mradi.
Akizungumza kwenye mkutano wa shina namba 5 katika Kijiji cha Hyadire, Chongolo amesema kuna baadhi ya viongozi wanachelewesha mambo ya maendeleo na kwa kuwa yeye ni katibu mkuu wa chama na ndiye bosi wa mawaziri wote hayupo tayari kuona mambo yanachelewa.
“Nimeongea na rais leo asubuhi, ameniambia niangalie maendeleo ya barabara hii, nitaenda kuchochea kwa rais kuwa waziri wake wa ujenzi ashughulika na barabara hii,” amesema Chongolo.