Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Daniel Chongolo amesema tabia ya wazazi na walezi Wilayani Morogoro kuwatumia watoto wa kike katika shughuli za kimila ikiwemo kucheza ngoma na kuwaozesha wakiwa bado na umri kinda kuwakosesha haki yao ya msingi ya kupata elimu.
Katibu Mkuu Daniel Chongolo amesema hayo baada ya kuwasili Wilayani Morogoro kutokea Wilayani Ulanga katika muendelezo wa ziara yake ya siku tisa ya kuimarisha chama Mkoani Morogoro.
Morogoro Wilaya yenye mila na desturi kama ilivyo maeneo mengine nchini lakini mila za wenyeji wa kabila la Waluguru zinadaiwa kuwa kikwazo kikubwa kwa mtoto wa kike kufikia malengo kielimu.