Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo ametoa siku 10 kwa Waziri wa Maji Jumaa Aweso kufika katika mradi wa maji katika kata ya Uhambingeto Wilaya ya Kilolo kusimama kwa zaidi ya miezi sita na kusababisha wananchi wa kata hiyo kutopata huduma ya maji ambapo walitakiwa kupata tangu mwezi wa tatu mwaka huu.
Ametoa maagizo hayo baada ya kufika kukagua mradi huo na kupokelewa na vilio vya kina mama na kukuta umefikia asilimia 55 ya utekelezaji wake huku mkandarasi Mshamindi Construction company limited akitafutwa anasema atafika lakini hafiki kwa mda wote huo ambapo ameagiza mpaka ifikapo mwezi wa tisa mwishoni maji yapatikane na kwa haraka anatoa Tank za plastic zisaidie upatikanaje kwa muda