Katibu wa Nec Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Sophia Mjema azungumza kuhusu mfumo wa M-Mama ambao umeanzishwa hapa nchini umesaidia kupunguza vifo vya akina Mama wajawazito wanapotaka kujifungua.
Mjema amesema hayo Mei 29,2023 alipokuwa akizungumza na wananchi baada ya kushiriki Mkutano Kwa Balozi wa Shina Na. 04 Kata ya Ifunda katika halmashauri ya wilaya ya Iringa akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa CCM ambaye yupo mkoani Iringa kwa ziara ya siku 7 ya kukagua uhai wa chama na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM.
Amesema Mkoa wa Iringa ni miongoni mwa mikoa ambayo mwaka huu 2023 wanatarajia kuanza kuanza kwa mradi huo wa M- Mama ambapo utakwenda kusaidia wanawake wengi wajawazito ili wasipoteze maisha wakati wa kujifungua.
Amewakumbusha wananchi wa Ifunda kuendelea kujikinga na maambukizi ya Virusi vya ukimwi kwa kuwa mkoa wa Iringa takwimu zinaonyesha maambukizi yapo juu.