Katika kuelekea Uchaguzi wa serikali za mitaa unaosimamiwa na TAMISEMI, unaotarajiwa kufanyika nchi nzima tarehe 27 Novemba mwaka huu, ambapo Watanzania watapata fursa ya kuwachagua Mwenyekiti wa Kijiji, Mwenyekiti wa Kitongoji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (Mchanganyiko) na Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (Kundi la Wanawake) watajwa kuwa utazingatia haki,haki na sheria .
Wakati huu Mitandao ya kijamii ni nyenzo muhimu ikiwa inatambulika kwamba wengi,inajikita kutoa taarifa sahihi na salama.
Lakini Mitandao ya kijamii pia imeleta ufahamu wa wajibu wa kijamii na haki za kijamii, hasa kwa vijana hivyo ni muhimu kuitumia kufanya vitu sahihi hasa tunapowasilisha mawazo kwani hii huweza kuzuia ufikiaji wa mitandao ya kijamii kwa usalama wa mtu binafsi taasisi mtu binafsi au taasisi.
Wakati tukielekea kwenye tukio hili muhimu ni vyema Serikali ikatambua ni umuhimu gani wa ufikiaji wa mtandao ili wananchi wapate taarifa kwa wakati hii ikijumuisha vyombo vya habari,redio,magazeti,blogs na wanaorusha maudhui moja kwa moja mtandaoni [online media]
Katika kuliona hilo kupitia kampeni ya #KeepItOnTZ, ambayo imeanzishwa na Zaina Foundation imehakikisha kwamba Serikali itaona maana ya kuzimwa kwa intaneti kunaweza kuwa na madhara makubwa katika ushiriki wa wananchi katika uchaguzi ujao.
Shirika la Zaina Foundation limejikita katika kuhamasisha wanawake juu ya matumizi salama ya mtandao likiamini kwamba matumizi ya intaneti ni haki ya msingi ya binadamu na ni moja kati mashirika machache yanayohimiza Serikali kutozima mtandao wa intaneti, kwenye kampeni yake ya #KeepItOnTZ kufikisha ujumbe .
Pia inasaidia jamii kujifunza juu ya kuzuia kuenea kwa taarifa potofu na kuhimiza ushirikiano kati ya vijana, wanajamii na vikundi katika mistari tofauti na kutambua fursa zilizopo ili kukuza amani.