Michezo

Kauli ya David De Gea kuhusu Manchester United na Real Madrid.

on

ddg

 

Habari ambazo mashabiki wa Manchester United wamekuwa wakihofia kuzipata hivi karibuni hatimaye zimekuwa kweli baada ya kipa namba moja wa klabu iyo Mhispania David De Gea kuiambia klabu hiyo kuwa anataka kuhamia Real Madrid .

De Gea kupitia wakala wake ameiarifu United kuwa dhamira yake ni kujiunga na Madrid na amefikia uamuzi huo baada ya kipindi kirefu cha kuwaza na kuamua ni hatua ipi bora ya kufuata kwenye mustakabali wake .

De Gea amekaa na United kwa muda wa miaka minne tangu aliposajiliwa toka Atletico Madrid kwa ada ya uhamisho ambayo iliweka rekodi kwa makipa ya paundi milioni 17 na amekaa United kwa muda wa miaka minne , muda ambao amepia hatua kubwa kiasi cha kufikia kuwa na kiwango cha ubora wa dunia .

Hivi karibuni De Gea alipewa ofa ya kuongezewa mshahara mpaka kufikia paundi 200,000 kwa wiki ofa ambayo hajaikubali akiwa amefikia uamuzi wa kurudi nyumbani kwao kwenye mji aliozaliwa na kukulia huku akipata fursa ya kuwa karibu na mpenzi wake Edurne .

De Gea amekuwa kwenye mipango ya Real Madrid kwa muda mrefu ambapo klabu hiyo imemuweka kama chaguo namba moja la kuziba nafasi ya mkongwe Iker Casillas ambaye umri wake unazidi kuwa mkubwa .

Endapo usajili huu wa David De Gea kuondoka United na kuhamia Hispania kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu , kipa huyo atakuwa mchezaji wa tano kuondoka United baada ya Cristiano Ronaldo , David Beckham , Ruud Van Nistelrooy na Gabriel Heinze.

Tupia Comments