Staa wa Yanga na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Farid Musa ameongea na AyoTV kwa mara ya kwanza kutokea Douala Cameroon na kueleza maandalizi ya timu kuelekea mchezo dhidi ya Guinea January 27.
Farid ambaye aliibuka Man Of The Match katika mchezo dhidi ya Namibia CHAN 2020 kwa kuifungia Tanzania goli pekee la ushindi wa 1-0 dakika ya 65 na kukufufua matumaini aeleza kuwa hilo limepita akili yao sasa ni mchezo ujao.