Michezo

Kauli ya Samatta baada ya mchezo wa Aston Villa dhidi ya Leicester City

on

Ni Headlines za  mtanzania Mbwana Samatta ambaye anatarajiwa kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza fainali ya michuano ya Carabao Cup nchini Uingereza itakayopigwa kwenye dimba la Wembley mnamo tarehe moja mwezi wa 3 baada ya hapo jana usiku klabu yake mpya ya Aston Villa kuwachapa Leicester City mchezo wa nusu fainali kwa mabao 2 – 1 na hivyo kujikatia tiketi ya kusonga mbele kwa idadi ya magoli 3 – 2.

Samatta kupitia ukurasa wake wa instagram aliyaandika maneno na kusema…“Nina furaha kwa ushindi wa jana usiku ikiwa ni mchezo wangu wa kwanza, Nashukuru kwa upendo mzuri kutoka kwa mashabiki, Tulicheza vizuri na Sasa tunaelekea Wembley”


Baada ya ushindi wa jana Aston Villa sasa kukutana kwenye mchezo wa fainali utakaochezwa tarehe 1/3/2020 katika uwanja wa timu ya taifa ya Uingereza Wembley jijini London.

 

Soma na hizi

Tupia Comments