Jina la Kobe Bryant ni moja ya majina ya mastaa wakubwa duniani ambao hata kama sio mfuatiliaji wa mchezo wa basketball, huenda ukawa unalifahamu pia.. uzito na ustaa wa jina lake ulifanya akawa mmoja wa mastaa wachache wanamichezo wanaofahamika zaidi duniani.
Kobe Bryant alianza kucheza kikapu mwaka 1996, baadae jina lake likaanza kupata headlines kubwa baada ya kupata kampani kubwa ya mkali mwingine, Shaquille O’Neal walipokutana kwenye kikosi cha Los Angeles Lakers….
Jina la Kobe lilikua sana na akawa anavunja rekodi kubwa zilizowahi kuwekwa na mastaa wengine ikiwemo Michael Jordan… umri wake umegusa miaka 37 kwa sasa na kaona kuna kila sababu ya yeye kustaafu.
Misimu miwili iliyopita ya Ligi ya Basketball Marekani NBA haikuwa na mazuri kwa Kobe kutokana na majeraha ya mguu na bega pia !!…
Msimu wa NBA unaoendelea sasahivi Kobe amesema utakuwa wa mwisho kumuona yeye uwanjani, miaka 20 aliyoitumia uwanjani imemtosha kabisa !!
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na MillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE