Top Stories

Agizo la Waziri Mwigulu kwa Polisi kuhusu kukamata wazururaji

on

Leo January 20, 2018 Waziri wa Mambo ya Ndani, Dr. Mwigulu Nchemba amelitaka Jeshi la Polisi nchini kutafuta namna ya kupunguza wahalifu wanaokamatwa kwa makosa kama uzururaji ili kupunguza mrundikano kwenye mahabusu.

Ameeleza kuwa suala hili pia litaepusha watuhumiwa wanaopelekwa mahabusu kwa makosa ya uzururaji kupata nafasi ya kuzungumzia masuala ya uhalifu na watuhumiwa waliozoea.

Kwa upande mwingine Dr. Mwigulu ameagiza wananchi kushirikiana na serikali katika ujenzi wa vituo vya polisi kwa kuwa suala la ulinzi ni ajenda ya kila Mtanzania na linapaswa kupewa kipaumbele.

Akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Dr. Mwigulu amesema kuwa mkakati wa Halmashauri hiyo kujenga kituo cha kisasa cha polisi ni kitendo cha kupongezwa kwani wanalenga kukomesha uhalifu wa aina zote.

CHADEMA yatangaza kugombea Kinondoni na Siha

Kifo cha Mama aliyegonga Ndege Airport Mwanza

 

Soma na hizi

Tupia Comments