Mix

Ripoti ya kinachoendelea Chuo kilichovamiwa Kenya.. Idadi ya vifo yaongezeka #RIP

on

Ke Attack

Hali bado sio shwari kwa wenzetu Kenya, jana taarifa kubwa iliyoripotiwa kwa siku nzima kutoka kwenye nchi hiyo ni ishu ya kuvamiwa kwa Chuo Kikuu cha Garissa, ambacho kiko karibu na mpaka wa nchi ya Somalia.

Wavamizi hao walivamia jana katika Chuo hicho na kuua walinzi wawili na baadae kuendelea kuwashambulia wanafunzi.

Idadi ya vifo iliyoripotiwa mpaka sasa ni watu 147, askari na Vikosi vya Jeshi la nchi hiyo wameendelea kuzunguka maeneo ya Chuo hicho.

Shambulio hili ni kubwa, linafananishwa na tukio la uvamizi wa Shopping Malls za Westgate, Nairobi September 2013 ambalo lilisababisha vifo vya watu 67 na wengine zaidi ya 170 kujeruhiwa.

Mpaka sasa wavamizi waliouawa ni wanne na mmoja wao amekamatwa.

.

Ramani ya Majengo ya Garissa University College.

Zaidi ya wanafunzi 500 walifanikiwa kutoka salama katika eneo hilo la Chuo.

Hii ni video iliyorekodiwa watu wakifanya jitihada za kukimbia kwenye mashambulizi hayo.

https://www.youtube.com/watch?v=JbOZ5Ye725M

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments