Mix

Saa ya mwisho baba anazungumza na mwanae alafu magaidi wako pembeni Kenya

on

A Kenya Defense Force soldier takes cover near the perimeter wall where attackers are holding up at a campus in GarissaKutokana na shambulio la kigaidi katika chuo cha Garissa kilichopo Kenya, baadhi ya familia bado hawajui watoto wao waliko, mzazi mmoja amesema aliongea na mtoto wake hadi dakika ya mwisho akiwa mikononi mwa magaidi hao baada ya kukamatwa.

Alikuwa akininong’oneza akiniambia yuko chini ya kitanda akaniambia tuu tumuombee akakata simu, saa sita na nusu nikaona hiyo namba ikinipigia nilikuwa naongea naye akaniambia nimeshikwa sina la kufanya akaniambia ndio hawa hapa silaha zao tunaziona, sijui ni bunduki sijui ni silaha gani walikuwa nazo..

Akaniambia ndio wanataka kuongea na baba lakini baba amepatikana wako busy sana wanamharasi, tukaongea nae kidogo wakamnyang’anya simu nikaongea na hao magaidi Al Shabaab …

Akiendelea kusimulia; “wakaniambia wee mzee nakupa dakika mbili apige Somalia, akaniambia wee mzee umeshindwa kupiga simu? Kama umeshindwa kupiga simu acha mwanao asali maombi yake ya mwisho mi nasikiliza tu.. akasali maombi yake yote akaniambia umesikia amemaliza kuomba what next we sikiliza, sikiliza mwenyewe hesabu mwenyewe risasi naua kabisa nikasikia three gunshot… na akaniambia nimeuwa chimbeni shimo”– aliongea mzazi wa mwanafunzi mmoja aliyeuawa.

Tukio hili limesababisha wanafunzi 147 kufariki na wengine kujeruhiwa, kwa sasa Chuo hicho cha Garissa kimefungwa kwa muda.

Pole kwa wote ambao wameathirika kutokana na tukio hili, #RIP watu wetu waliofariki.

Sikiliza taarifa hiyo hapa iliyoripotiwa na kituo cha K24 kwa kubonyeza play…
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments