Stori Kubwa

Taarifa kubwa kutoka Kenya zilizosikika kwenye #countdown ya Amplifaya leo Jan 5 (Sauti & Video)

on

Nairobi-City

Walimu saba raia wa Kenya wamejeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara Somalia, mtu mmoja alifariki kutokana na mlipuko huo uliokuwa umelenga basi la shule.

Watu watatu wamefariki na majeruhi wametajwa kuongezeka kutoka na kuanguka kwa jengo la ghorofa saba huko Nairobi, Mkurugenzi wa CID Ndegwa Muhoro ameagiza wahusika wote kujisalimisha kituo cha Polisi.

Rais Uhuru Kenyatta ameitembelea familia ya Raila Odinga kuwapa pole ya kufiwa na mtoto wa kwanza wa Odinga, Fidel Odinga ambaye alifariki usiku wa kuamkia jana Jumapili katika mazingira ya kutatanisha nyumbani kwao.

Unaweza kusikiliza taarifa zote katika sauti hii kwa kubonyeza play.

Ile taarifa ya ghorofa kudondoka iko hapa pia, unaweza kuitazama.

Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments