Stori Kubwa

Taarifa ya mashahidi wanne kesi ya William Ruto waliopotea, pamoja na mmoja aliyeuawa.

on

TZA-KE.UKURASA WA KWANZA STAR YA LEO. (1)

Ukurasa wa mbele wa Gazeti la The Star, Kenya.

Taarifa kutoka Kenya zinasema mashuhuda wengine wanne wa kesi ya inayomkabili Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto katika Mahakama ya ICC wamepotea katika kaunti ya Uasin Gishu, Kenya.

Hili limetokea siku chache baada ya shahidi mwingine Meshack Yebei kuuawa katika mazingira ya kutatanisha, huku ndugu wakisisitiza kutaka kufanya mazishi ya mtu huyo kinyume na uamuzi wa Mawakili wa William Ruto ambao wanataka mwili huo ufanyiwe uchunguzi kwa kuwa marehemu alikuwa mmoja ya mashahidi muhimu wa kesi hiyo.

Mwanaharakati wa Haki za Binadamu Kenya, Ken Wafula amewataja mashuhuda wa kesi ya Ruto waliopotea ni  Yohana Kimng’etich Bureti, Benjamin Kipchumba, Phillip Arusei na mwingine aliyetambulika kwa jina moja la Miriam.

Watu mbalimbali pamoja na Wabunge wa Jubilee wamemtaka Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Kenya kumchunguza Wafula wakimtuhumu kuhusika na tukio la mauaji ya Yebei, huku Wafula naye akiishitumu Serikali kuhusika na matukio ya mauaji na upoteaji wa watu hao.

 Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments