Imetimia miaka kumi tangu moja ya shambulio baya kuliko yote nchini Kenya, lililouwa watu 67 na kujeruhi wengine 200 katika eneo la maduka la westgate katika mji mkuu wa Nairobi Septemba 20, mwaka 2013.
Ilikuwa Jumamosi mchana wakati watu wenye silaha walipo vamia eneo hili la maduka lililokuwa limejaa watu na kuanza kushambulia kwa bunduki za rashasha na kurusha magruneti.
Watu hao wenye silaha walilishikilia eneo hilo kwa takriban saa 80, kabla ya vikosi vya usalama kuchukua udhibiti.
Miaka kumi baadaye, Loi Awat bado anakumbuka maombi ya kukata tamaa ya watu waliokuwa karibu naye wakati alipokuwa ameshikiliwa kwa siku nne katika eneo la maduka ya kifahari la Westgate.
Kwa saa nne za kutisha, Awat alijikunja chini ya meza ndogo katika ukumbi wa benki kwenye eneo hilo la maduka jijini Nairobi, ambako alikwenda kutoa pesa kwa ajili ya kuhudhuria mchezo wa rugby na binamu zake wawili.
Baada ya shambulio hilo, Kenya imeshuhudia mashambulio mengine likiwemo shambulio kwenye chuo kikuu cha Garissa ambapo wanafunzi zaidi ya mia waliwauwa,shambulio la hotel ya Dusit mwaka 2019 watu 21 wakiwauwa.
Maeneo ya kaskazini mashariki na Pwani ya Kenya, haswa Lamu bado yameendelea kulengwa na Al Shabab hadi sasa, hatua ambayo imemlazimu waziri wa usalama wa ndani Kithuri Kindiki kutangaza kuwatuma vikosi maalum maeneo hayo.
Kenya iliamua kuwatuma wanajeshi Wake nchini Somalia mwaka 2011, uamuzi ambao umeifanya kuwa shabaha ya Al Shabab.