Shirikisho la Soka barani Afrika Jumatano lilizipa Kenya, Uganda na Tanzania haki ya kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika 2027.
Rais wa CAF Patrice Motsepe alitangaza Zabuni ya Pamoja ya Afrika Mashariki kama mshindi wa haki za kuandaa bonanza la kwanza la kandanda la Afrika baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji ya CAF mjini Cairo, Misri.
“Mustakabali wa soka wa Afrika haujawahi kuwa angavu zaidi na katika siku za usoni taifa la Afrika litashinda Kombe la Dunia,” Motsepe alisema.
Mataifa ya Afrika Mashariki yaliwashinda Misri, Senegal, Botswana na Algeria – ambao walijiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho siku mbili kabla ya kutangazwa rasmi – kwa haki za kuandaa.
Tazama pia ….