Wanafunzi 14 wamefariki dunia huku wengine 39 wakijeruhiwa katika Shule ya Msingi Kakamega nchini Kenya kutokana na kukanyagwa na wenzao na kuanguka wakati wakikimbia.
Ajali hiyo imetokea Jumatatu February 3 majira ya saa 11 joni wakati watoto hao wakitoka madarasani kurejea makwao, ambapo tayari wanafunzi 20 waliojeruhiwa wameruhusiwa kutoka hospitali. “Kumpoteza mtoto ni tukio linalouma sana. Natoa salamu za pole kwa wazazi wote waliofiwa na watoto wao,” Waziri wa Elimu, George Magoha amesema.
Kamanda wa Polisi wa Kakamega, David Kabena amesema chanzo cha tukio hilo hakijafahamika lakini amebainisha kuwa tayari uchunguzi umeanza.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wanasema watoto walikuwa wakiteremka ngazi wakikimbia baada ya kumaliza vipindi vya siku, ndipo ngazi hiyo ilipovunjika, na kusababisha baadhi ya wanafunzi kuanguka kutoka ghorofa ya tatu.
TRA FUTILIA MBALI MAWAKALA WA EFDs “MIEZI MITATU HAWAJANIPA MASHINE”