Sikukuu ya Madaraka ya mwaka 2023 ni sherehe ya kitaifa ya kwanza kufanyika nje ya Nairobi tangu Rais William Ruto achukue madaraka.
Sikukuu ya Madaraka inasherehekewa na wakenya kama ukumbusho wa wakati ambao nchi yao ilipata madaraka mnamo wa mwaka wa 1963 kutoka kwa waingereza na husherehekewa kila tarehe 1 mwezi wa sita kila mwaka na hii leo raia wa Kenya wanaadhimisha miaka 60 tangu waasisi wa taifa hilo walipokabidhiwa madaraka kutoka kwa mkoloni na kuunda Serikali ya kwanza ya Kenya.
Hatahivyo siku hii inaadhimishwa huku raia wa nchi hiyo wakikumbwa na hali ngumu ya kiuchumi inayotokana na mfumuko mkubwa wa bidhaa muhimu kama vile chakula la mafuta.
Raia pia wamelalamikia pendekezo la rais wa nchi hiyo William Ruto ya kukatwa kwa mishahara ya wafanyakazi nchini humo kwa 3%, ili kufanikisha utekelezaji wa sera ya serikali ya ujenzi wa makazi kwa raia wenye kipato cha chini.
Sherehe za kitaifa za Madaraka Day zinafanyika katika Kaunti ya Embu nchini humo, ambako rais William Ruto anatarajiwa kutoa hotuba maalum ya siku hii, huku Wakenya wakisubiri ni nini atakalosema kuhusiana na kupanda kwa gharama ya maisha.