Michezo

Pale ambapo viatu vimesababisha Mwanariadha wa Kenya ashindwe kuvunja Rekodi ya Dunia..

on

Eliud Kipchoge ni Mwanariadha aliyewakilisha Kenya kwenye Mashindano ya Riadha ya Berlin Marathon ambayo yamefanyika Berlin Ujerumani… Round ya kwanza haikuwa na neema kwake, ulimi wa ndani ya viatu ulitoka na kusababisha jamaa ashindwe kuivunja Rekodi ya Dunia kwenye Mashindano hayo.,

Unaweza kuchukulia ni kitu cha kawaida, lakini Eliud anasema mpaka anamaliza mbio alikuwa na malengelenge miguuni pamoja na kidole gumba kupata jeraha na kutokwa damu nyingi, hiyo ilifanya amalize round zote za Riadha akiwa na wakati mgumu sana !!

A_Nike_runner_missed_a-0393ac16366df7c6748c4ae43dd0b500

Haikuwa siku nzuri mimi kutumia hivi viatu, nilivijaribu nikiwa Kenya na vilikuwa sawa tu!! Lengo langu ilikuwa nivunje Rekodi ya Dunia leo lakini naona haikuwa siku yangu– Eliud Kipchoge.

Mbali ya changamoto zote, Eliud aliibuka na ushindi kwenye mbio za Maili kumi huku akiweka Rekodi ya kumaliza mbio kwa saa mbili na dakika nne.

Unaweza kucheki kwenye hii video ya sekunde 76 mbio zenyewe ilivyokuwa mpaka mwisho…

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Tupia Comments