Habari za Mastaa

Good news… Navy Kenzo Feat. Vanessa Mdee imegusa hapa kwenye Countdown ya Radio Nigeria…

on

Navy Kenzo Game

Siku zote huwa nafurahishwa sana pale ninapoona watu wangu kutoka Tanzania wanazidi kufanya vizuri kimuziki, sio siri wasanii wetu wanafanya sana kazi na kwa bidii, kazi ambazo zinapata mapokezi mazuri kwenye countdown mbalimbali za radio Africa.

iika

Good news kwako mtu wangu wa nguvu, nimepita kwenye mtandao wa Twitter na nimekutana na post ya @The Beat 99.9 FM ya Lagos Nigeria na kwenye #AfricanTop10 countdown yao wimbo kutoka Tanzania ‘Game’ wa watu wetu Navy Kenzo waliomshirikisha Vanessa Mdee umeshika nafasi ya #1 wiki hii.

vee

Hii ni good news sana na kusema kweli inafurahisha sana, Watanzania wanazidi kupenya kwenye soko la muziki Nigeria na sehemu mbalimbali Africa, ilianza ya Vanessa Mdee ‘Nobody but me’ sasa ni zamu ya Navy Kenzo kuipeperusha code ya #255.

the beat

Hapa chini nimekuwekea video yao mtu wangu karibu uitazame.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments