Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM), Masumbuko Mgaya ameachiwa na Polisi kwa dhamana ikiwa ni baada ya Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma, Gilles Muroto kusema hana taarifa za kukamatwa kwa Mwanafunzi huyo.
Taarifa ya kuachiwa imetolewa na Uongozi wa Chuo hicho kupitia Ofisi ya Uhusiano wa Umma na Masoko ambapo awali Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Faustine Bee amesema Mgaya alishikiliwa kwa makosa matatu ya matumizi ya mbaya mtandao.
Alikamatwa Januari 21 na wenzake wanadai walifika Kituo cha Polisi lakini hawakufanikiwa kumuona na kuambiwa amepewa dhamana lakini hakuonekana Chuoni na wala alikuwa hapatikani kwenye simu.