Baada ya watu wengi kulalamika juu ya uongozi wa klabu ya Simba kuamua kutangaza kumtimua aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo muingereza Dylan Kerr, usiku wa January 18 mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Haji Manara ameweka wazi jambo lililomfanya kocha huyo aondolewa ndani ya Simba.
Manara amefunguka akiwa katika kipindi cha Sport Bar cha Clouds Tv kuwa uongozi uliamua kukaa kimya tu, kwani hawakutaka kusema chochote, ukweli Kerr ana matatizo yaliompelekea kuondolewa Simba, kwanza Kerr hashauriki na mtu yoyote, pili timu haina first eleven hadi leo toka ameanza kuifundisha miezi sita nyuma la tatu ni kuwa watu wanataka timu ipate matokeo. Hivyo ni ngumu kufanya kazi na kocha wa aina hii.
“Kerr watu wanalalamika hawajui mimi nizungumze moja tu, miezi sita sasa Simba haina first eleven, halafu Kerr hana anayemshauri sio uongozi wala makocha wenzie, mfano mimi nilikuwepo Zanzibar nilipomtambulisha Mayanja akasema huyu namjua mafya sana nimepata habari zake, hivi kweli mgeni ndio unampokea hivyo? ” >>> Manara
Unaweza msikiliza Manara katika mahojiano na Sports Bar ya Clouds Tv
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.