Habari za Mastaa

Kesi ya Asap Rocky yamfikia Rais Donald Trump

on

Baada ya mwanadada Kim Kardashian pamoja na mumewe Kanye West kufanya mahojiano na mkwe wa Rais Donald Trump kuhusu kesi inayomkabili Rapper Asap Rocky ambaye yupo jela nchini Sweden, sasa hatimaye Donald Trump taarifa hizo zimemfikia.

Imeripotiwa kuwa Rais Donald Trump amezungumza mbele ya vyombo vya habari kuhusiana na taarifa za rapper huyo na kusema kuwa tayari ameshafanya mazungumzo na Kanye West jinsi ya kumsaidia Asap na atafanya mawasaliano ya simu na Waziri Mkuu wa Sweden kuona ambacho kinaweza kufanyika.

“Nimeongea na Kanye West kuhusu rafiki yake Asap Rocky ambaye amefungwa, nitampigia Waziri Mkuu wa Sweden nione tutakachoweza kufanya kuhusu kumsaidia Asap Rocky, najua watu wengi wanataka kuona hii ishu ikitatuliwa haraka”>>> aliandika Rais Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter

Asap Rocky anashikiliwa na polisi nchini Sweden tokea July 3,2019 kwa tuhuma za kumpiga shabiki mmoja kwenye mitaa ya Stockholm huku sababu kubwa ya ugomvi huo ukitajwa kuwa ni headphones za Asap ambazo zilidaiwa kuharibiwa.

PART 3: ZARI KAELEZEA MATUMIZI YA WATOTO, KUMBLOCK BABA WATOTO WAKE “MOYO ULINIUMA”

Soma na hizi

Tupia Comments