Rapper wa kike kutokea nchini Marekani , Cardi B ametoa ushuhuda katika Mahakama ya Georgia State akimshtumu mmiliki wa channel ya Youtube nchini humo.
Cardi B amemfikisha Mahakamani Tasha K kwa kumshtumu kusambaza habari zisizo za kweli.
Kwa upande wa Cardi b alieleza Mahakama kwamba amekuwa akishindwa kulala na kutoelewana na familia yake kutokana na habari zilizokuwa zikiandikiwa katika mtandao huo.
Mahakama ilipomsikiliza Tasha K alikanusha taarifa hizo na kesi hiyo imeahirishwa kusikilizwa tena mnamo Januari 18,2022.
AUNT EZEKIEL AANGUA KILIO MAHAKAMANI, KESI YA DAWA ZA KULEVYA “SAID MBASHA NA WENZAKE”