Mkuu wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, (RPC) Ramadhan Kingai amekana kumtesa mshitakiwa Adam Kusekwa kabla na baada ya kuandika maelezo yake ya onyo kama upande wa utetezi unavyodai.
Kingai ameeleza hayo katika Mahakama Kuu Kitengo cha Makosa ya Uhujumu uchumi mbele ya Jaji Mustafa Siyani, wakati wa usikilizwaji wa kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi wakipinga kupokelewa kwa maelezo ya onyo ya mshitakiwa huyo.
Hatua hiyo imekuja baada ya Upande wa Utetezi ukiongozwa na Wakili Peter Kibatala kupinga mahakama isipokee maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili ambayo yalipaswa kutolewa mahakamani hapo kama kielelezo na shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka ambaye ni Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kinondoni, RPC Ramadhani Kingai.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho Septemba 16, 2021 ambapo Kingai ataendelea kutoa ushahidi akiwa ni shahidi wa 7 katika kesi ndogo baada ya ile ya msingi kusimama.
KESI YA MBOWE: KAMANDA KINGAI AKANA KUMTESA KOMANDOO MSTAAFU, MAPYA YAJITOKEZA