Top Stories

Kesi ya Mbowe yaahirishwa kwa Dakika 45

on

Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imeahirisha kwa muda wa dakika 45 kesi ya Ugaidi na Uhujumu Uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake.

Kesi hiyo ilikuwa ikiendelea na usikilizwaji wa shahidi wa tatu Askari Polisi, H 4323 Msemwa mbele ya Jaji Mustafa Siyani ambapo shahidi huyo alikuwa akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi Nassoro Katuga.

Jaji Siyani ameahirisha kesi hiyo kwa dakika hizo ili kutoa nafasi kwa watu wote waliopo chumba cha Mahakama kupata mapumziko mafupi kabla ya ushahidi kuendelea.

Washitakiwa wengine katika kesi namba 16/ 2021 ni Halfan Bwire, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Lingwenya.

LIVE: ASKARI ALEMUUA HAMZA ANASIMULIA

Soma na hizi

Tupia Comments