Aliyekuwa mkuu wa wilya ya Hai Lengai Ole Sabaya anayetuhumiwa kwa kosa la Unyang’anyi wakutumia Silaha akiwa na wenzake wawili ameanza kujitetea nakusema bado yeye ni mtumishi wa Serikali na kwamba aliagizwa na aliyemteua kwenda kwenye duka lililopo mtaa wa soku kuu Arusha
Akiongozwa na wakili wa utetezi moses mahuna mbele ya hakimu Orira Amworo amesema aliteuliwa na aliyekuwa rais wa Tanzani hayati Dkt.Jonh Pombe Magufuli ambapo alikuwa chini ya kiapo cha utii wa katiba kutotoa siri yeyote anayoifahamu katika majukumu yake ila tu idhini ya Rais aliyemteuwa pekee.
Amesema Utumishi wake wa ukuu wa wilaya ulikoma May 12 2021 baada ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kutoa taarifa hiyo ya kumsimamisha ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zilizokuwa zikimkabili lakini kwa mujibu wa sheria za Utumishi wa umma bado ni yeye mtumishi wa Serikali.
Sabaya anasema February 2 2021 akiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai aliongoza kikao cha kamati ya ulinzi na usalama katika wilaya ya Hai.Sabaya amesema hawezi kueleza Mahakamani hapo kilichokuwa kinajadiliwa kwenye kikao hicho kwa kuwaa ni siri.
Sabaya amesema majira ya saa tisa kasorobo alipokea simu kutoka kwenye mamlaka iliyomteua nakumpa maelekezo kuna watu wameshuka uwanja wa KIA uliopo wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro na kwamba wanapaswa kwenda nao Arusha.Sabaya anasema baada yakuwachukua watu hao walipanda kwenye gari lake nakuongozana nao wakiwa na Magari mawili kuelekea mkoani Arusha kwa kuwa walikuwa tayari wameshapatiwa taarifa zote na kwamba walikuwa na watu wanne
Baada ya kufika Arusha walienda eneo husika la soko kuu walilokuwa wamepangiwa na walipofika hawakumkuta waliokuwa wakimtafuta ambapo walifanya mawasiliano na mamlaka iliyowapa maelekezo ambapo baadaye mamlaka ikamuambia wameshawasiliana na aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi nakutakiwa kuwachukua watu hao kuwapeleka kituo cha polisi ili kuwezesha upatikanaji wa mtu huyo waliyekuwa wakimtafuta anayefahamika kwa jina la Mohamed Saadi Hajirin
Sabaya anasema aliwachukua watu hao baada yakufunga dula lao huku mali zao zikiwa salama nakuhakikisha nakuwapeleka kituo cha polisi nakuwakabidhi nakuwaambia maelekezo mengine tayari ameshapewa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi
Sabaya amesema hawezi kuwakumbuka kwa majina aliowapeleka polisi na hawakuwa wamiliki wa duka hilo bali ana fahamu kuwa wana mahusiano na aliyekuwa akitafutwa.
Sabaya amesema hawezi kuwataja watu aliokuwa nao kwa sababu ilikuwa kazi maalumu na ndio maana wengine hawapo kwenye shtaka hilo.Sabaya amesema anapopewa kazi ya namna hiyo huwa anashirikiana na Vyombo vyote vya dola vya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Sabaya amesema anayeweza kufahamu kwa nini alitumwa Arusha ile hali kuna polisi,TAKUKURU na Uongozi ni mamlaka iliyomtuma kwa kuwa si mara ya kwanza kwani miezi michache iliyopita alitumwa kufanya Operesheni yakukamata mitambo
Anasema walifanikiwa kukamata mtambo wakutengeneza noti bandia eneo la Chanika Dar na Gavana wa benki kuu anafahamu na waziri wa fedha kwa kipindi hicho ambaye ni makamu wa Rais wa sasa anafahamu suala hilo.Sabaya amesema asingeweza kuibishia mamlaka hiyoo kwa kuwa ilimpa kazi nyingine yakufuatilia kampuni ya Q Net mkoani Mwanza ambayo ilikuwa inachukua Fedha za waalimu kwa madai yakupanda mbegu.
Sabaya amesema shtaka la Unyang’anyi wakutumia silaha inayomkabili Lengai Ole Sabaya katika mtaa wa bondeni sio la kweli kwa kuwa tarehe 9 2.2021 hakufika eneo hilo na hakuwa na mshtakiwa wa pili na watatu ambao wanashtakiwa nao kwenye kesi hiyo.
Sabaya amesema hawafahamu kabisa mshtakiwa wa tatu Daniel Mbura na hajawahi kuwaona kabisa na fedha hizo milion mbili laki saba na elfu sitini na saba elfu zilizoandikwa kwenye shataka hazifahamu na wala hajawahi kuziiba na hakuna shahidi yeyote kati ya 11 aliyesema alimuona akiwa anaiba fedha.
Amesema mashahidi waliofika mahakamani hapo wamesema tarehe 12 2 2021 waligundua wizi wa mashine za EFDS na nyaraka nyingine na hakuna sehemu waliposema tarehe 2 February.
Sabaya amesema hamfahamu Mohamed Saadi Hajirin aliyetajwa mahakamani hapo na hajawahi kumuona akisema aliibiwa fedha ila Anayefahamika kwa jina la Mohamed Saadi ambaye ametajwa kwenye hati ya mashtaka hajawahi kumsikia akisema aliibiwa fedha hizo na hakuna shahidi yeyote aliyeleta kielelezo mahakamani kikionyesha fedha hizo ziliibiwa.
Sabaya amesema mashahidi walioletwa na Jamhuri Noman saadi na wengine waliodai kutishiwa na silaha ili watoe fedha amesema hakuna sehemu aliyosema alimuona mtu kama yeye akiina Fedha.
Sabaya amesema maelezo ya mkuu wa upelelezi wa Wilaya ya Arusha Venance Bakwisa yana mashaka kwa kuwa alisema alitoa p3 mbili ile hali p3 iliyoletwa Mahakamani ni moja ya diwani wa SOmbetini Bakari Msangi.
Sabaya amesema hajawahi kukutana na bakari msangi popote na wala hajawahi kumpiga lakini anamfahamu kwa kuwa mwaka 2017 Februari aligombea naye nafasi ya Mwenyekit wa UVCCM Mkoa wa Arusha ambapo alimshinda yeye na wenzake na baada ya hapo alimteua kuwa mjumbe wa baraza hilo la vijana kwenye mkoa wa Arusha.
Amesema bakari waliungana na kundi lililokiwa na uchu na mali ya chama nakutengeneza mgogoro wa kisiaasa nakupelekea kupelekwa mahakamani na baadaye rais kuunda tume na kesi hiyo kufutwa na DPP.
Amesema siku ya tukio tarehe 9 mwezi wa 2 hajawahi kumpiga wala kukutana naye popote na maelezo ya mke wa Msangi yanatofautiana na ya Bakari kwa kuwa Bakari anadai alikuwa na laki nne akanunua mapapai ya shilingi elfu 10 akabakiwa na laki tatu na tisini lakin mke wa bakari anadai alikuta mapapai mawili tu nakubakisha laki tatu na tisini na tano tu.
Sabaya amesema ana miliki silaha na siku ya tukio aliacha boma ngombe na hajawahi kuitwa kuhojiwa polisi kuhusu silaha anayomiliki na wala hajawahi kupekuliwa nyumbani.
Sabaya amesema kwenye hati ya mashtaka anashatakiwa kwenda mtaa wa bondeni kuibia watu lakini mashahidi wanazungumzia tukio hilo limefanyika kwenye duka.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 16 2021 ambapo shahidi huyo ambaye ni mshtakiwa namba moja ataendelea kutoa ushahid wake.