Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma imeahirisha kesi namba 23627 ya mwaka 2024 ya kubaka kwa kundi inayomkabiri Fatmah Kigondo ‘Afande’ baada ya Hakimu Francis Kishenyi kubadilishiwa kituo cha kazi.
Shauri hilo lililofungulia na wakili Paul Kisabo lilianza kusikilizwa Agosti 23,2024 kabla ya kuahirisha hadi leo Septemba 05,2024 ambapo shauri hilo limeahirishwa hadi Octoba 07,2024
Nje ya mahakama tumempata wakili Paul Kisabo ambaye ndiye aliyefungua shauri hili amesema “Tulipofika hapa mahakamani tumepewq taarifa kuwa hakimu Francis Kishenyi amehamishwa kituo cha kazi kwahiyo shauri limeahirishwa mbele ya mheshimiwa Tungalaja na mamlaka katika shauri hili ni kuahirisha tu kwasababu shauri hili halijapangiwa hakimu wakulisikiliza na siku ya leo Fatmah Kigondo alifika mahakamani hivyo shauri limeahirishwa hadi tarehe 07-10-2024 katika mahakama hii ya hakimu mkazi Dodoma tunaamini siku hiyo tutakuta shauri limepangiwa hakimu wa kulisikiliza” Paul Kisabo